Dodoma FM

Ujenzi wa Tenki kupunguza adha ya maji Mahunga

14 September 2026, 15:55

Picha ni Tenki la maji ambalo limejengwa kwaajili ya kuhifadhia maji.Picha na Dima online.

kukamilika kwa Tenki la maji kupitia mradi wa kisima cha Mahunga hivyo kuanza kutoa huduma kwa vijiji vya Mlowa barabarani na Mlowa B.

Na Victor Chigwada.

Kukamilika Kwa Tenki la maji lililokuwa likijengwa katika kitongoji cha Mahunga Kata ya Mlowa barabarani kutasaidia kupunguza kero ya upungufu wa maji katika eneo hilo.

Hayo yanathibitika na baadhi ya wakazi wa Mlowa B ambao  ni miongoni mwa wanufaika wa  mradi huo ambapo wamesema kukamilika kwa Tenki la kuhifadhia maji kutasaidia upatikanaji wa maji kuwa rahisi.

Anjero Lukasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani amekiri kukamilika kwa Tenki la maji kupitia mradi wa kisima cha Mahunga hivyo kuanza kutoa huduma kwa vijiji vya Mlowa barabarani na Mlowa B,

Aidha ameongeza kuwa kukamilika Kwa mradi wa Mahunga lakini bado usambazaji wa miundombinu majumbani bado haujaanza huku suala la uhaba wa maji kutokana na namba ya wakazi wa Kata yake

Ripoti na Victor Chigwada.