Dodoma FM
Dodoma FM
12 December 2025, 16:06

Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Alhaj Jabir Shekimweri katika ziara ya Mafunzo ya Mnyororo wa Ugavi wa Dawa. Picha na Lilian Leopold.
Katika hatua ya mwisho ya ziara hiyo, viongozi hao wamewahimiza watumishi wa sekta ya afya kuendelea kushirikiana, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha upatikanaji wa dawa pamoja na huduma nyingine muhimu unaboreshwa ili kwenda sambamba na mabadiliko na ongezeko la watu katika jiji la Dodoma.
Na Lilian Leopold.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri amewataka watumishi wa afya katika hospitali ya jiji iliyopo Nala jijini Dodoma kuendelea kuboresha utendaji wao wa kazi, akisema jiji la Dodoma linakua kwa kasi huku serikali ikiendelea kuboresha miundombinu ya afya katika hospitali hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo jumuishi.
Shekimweri ameyasem hayo katika ziara ya Mafunzo ya Mnyororo wa Ugavi wa Dawa, iliyohusisha ukaguzi wa ukaguzi wa kituo cha afya Makole na Hospitali ya jiji, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wahudumu wa afya kwa kujitoa kwako katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi amewataka watoa huduma za afya kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia maadili ya kazi na kutanguliza maslahi ya wananchi wanawahudumia.
Aidha baadhi ya watoa huduma ya afya walioshiriki katika ziara hiyo akiwemo Mganga mkuu jiji la Dodoma Daktari Pima Sebastian na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Makole Revocatus Baltazary wamesema kuwa wanajitahidi kutoa huduma bora na kuahidi kuongeza juhudi ili kukidhi mahitaji ya wananchi.