Dodoma FM
Dodoma FM
29 April 2026, 17:13

Aidha Ndalu ameongeza kuwa ni vyema Wizara ya ardhi kupitia kampuni iliyopewa dhamana kukamilisha zoezi hilo kwa maslahi ya wananchi.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Mahata Kijiji cha Chinangali II wameiomba Serikali kusimamia kwa karibu zoezi la urasimishaji wa ardhi lililo kuwa limeanza katika maeneo yao lakini limeshindwa kukamilika katika baadhi ya vitongoji.
Wakiongea na Taswira ya Habari wananchi hao wamesema wanaiomba serikali kukamilisha zoezi hilo ili kila mwananchi mwenye ardhi apate hati ya umiliki wa ardhi na kuepusha migogoro ya ardhi.
Mwenyekiti wa kijiji cha chinangali ii Bw.Yuda Ndalu amekiri uwepo wa changamoto ya ujenzi na shughuli mbalimbali katika maeneo ambayo tayari yamesha rasimishwa ingawa bado hayana alama za kuonyesha mipaka hususani miundombinu ya barabara