Wazazi na walezi waongoza ukatili kwa watoto Dodoma
22 May 2026, 18:05

Kwa upande mwingine Afisa huyo amewashauri wazazi kuzingatia adhabu wanazotoa kwa watoto wao ili kuto leta madhara zaidi kwani kutoa adhabu zisizo faa kwa watoto ni kukiuka haki zao na kuvunja sheria.
Na Jerome John.
Imeelezwa kuwa wazazi na walezi wanaongoza kwa kufanya vitendo vya ukatili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka minane katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Akizungumza naTaswira ya Habari Rosemary Nicodemas Afisa Ustawi wa jamii jiji la Dodoma amesema kuwa kulingana na taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto katika jiji la Dodoma wazazi ndio wamebainika kufanya ukatili huo kwa watoto wao.
Aidha bi,Rosemary amesema kuwa watoto hao wamekuwa wahanga kutokana na kutokuwa na uwezo wa kujitetea wanapo kuwa wakifanyiwa ukatili huo kwa njia ya kupigwa kupitiliza,kuchomwa moto mikono au kumwagiwa maji ya moto pamoja na kufungwa mikono au miguu.
Afisa ustawi huyo amebainisha kuwa wazazi hufikiri kuwa kutoa adhabu hizo ni njia ya kuwafundisha watoto kumbe ni kuwaumiza zaidi au kuwapatia majeraha ya mwili mojakwamoja.