Dodoma FM

Magufuli atakumbukwa kwa utendaji wake

26 March 2021, 11:52 am

Na; Mariam Kasawa.

Hayati Dkt.John Pombe Magufuli atakumbukwa kwa  utendaji kazi wake kwani alikuwa hodari tangu akiwa Waziri hadi  alipoteuliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika tukio la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli wilayani Chato Mkoani Geita.

Mhe.Dkt.Kikwete amesema Magufuli alikuwa kati ya  Mawaziri aliowaamini na kuwatumaini ndio maana alimuweka kwenye Wizara tatu zilizokuwa ngumu.

Amesema katika mchakato wa kupitisha majina ya wagombea Urais 2015 hakuweza kusita kulichagua jina la Rais Magufuli kwani alifahamu fika utendaji wake wa kazi.