Dodoma FM

Wafanyabiashara wakiri biashara kuwa ngumu msimu huu wa sikukuu

19 December 2023, 6:41 am

Picha ni eneo la onewey jijini Dodoma eneo maarufu kwa bishara ya nduo na viatu.Picha Aisha Alim,

Watu wanashauriwa kufanya maandalizi mapema ya mahitaji kwa ajili ya kipindi cha sikuku ili kuepuka uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo bidhaa kupanda bei.

Na Aisha Alim.

Wafanyabiashara wa nguo pamoja na mapambo ya christmas katika eneo la one way Jijini Dodoma wameeleza kuwepo kwa ugumu wa biashara hasa katika kipindi hiki kuelekea sikuu za mwisho wa mwaka tofauti na miaka mingine

Picha ni mfanyabiashara wa mapambo akiongea na Dodoma Tv .Picha na Aisha Alim.

Wakizungumza na Dodoma Tv wafanyabiashara hao wamesema hali ya biashara hairidhishi tofauti ni misimu mingine ya sikukuu kwani kumekuwa na mwitikio mdogo wa wateja kupata mahitaji yao.

Sauti za wafanyabiashara.

Nao baadhi ya wateja akiwemo Bi. Zulfa kassidi amesema wamejiandaa mapema kuelekea sikuu za mwisho wa mwaka lakini kutokana na bei kubwa ya bidhaa wanashindwa kukidhi mahitaji yao.

Sauti za wanunuzi