Dodoma FM

Unakabiliana vipi na kupanda kwa gharama za maisha?

8 May 2026, 17:27

Mambo matatu makubwa yanayowaumiza wananchi ni kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa ajira na kipato na uhaba wa chakula.Picha na mtandao.

Utafiti wa Twaweza, ulifanyika katika mikoa ya Tanzania ikiwemo Dar es Salaam, katika maeneo ya mijini na vijijini na kuwahoji wananchi kuhusu nini mahitaji yao kwa serikali za mitaa na wananchi hao walilalamikia huduma za afya, upatikanaji wa maji safi, huduma duni za usafiri na ubora wa elimu.

Na Mariam Kasawa.

Mnamo mwaka 2022 Utafiti wa ‘Sauti za Wananchi’ nchini Tanzania unaoangazia gharama za maisha na tozo uliebaini kuwa wananchi wengi walikuwa na wasiwasi na kupanda kwa gharama za maisha, ajira, fursa za kipato na uhaba wa chakula.

Utafiti huo uliozinduliwa jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Twaweza, ulionesha kuwa, mambo matatu makubwa yanayowaumiza wananchi ni kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa ajira na kipato na uhaba wa chakula.

Katika utafiti huo, asilimia 56 ya watu waliohojiwa, walilalamikia kupanda kwa gharama za maisha na asilimia 50 walilalamika kukosa ajira na fursa za kipato na asilimia 27 walilalamika njaa na uhaba wa chakula.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema matokeo yaliyomshangaza katika utafiti huo ni wasiwasi wa chakula kwa watu wa vijijini.