Dodoma FM

Wananchi waomba kupatiwa elimu ya uwekezaji

24 April 2023, 2:26 pm

Wakazi wa Jijini Dodoma wakiendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiingizia kipato.Picha na Thadei Tesha.

Mara kadhaa vijana wamekuwa wakilalamikia kukosa fursa za kujikwamua kiuchumi ambapo moja ya changamoto kubwa ni ukosefu wa elimu juu ya kuzitambua fursa hizo.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wameiomba serikali kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini pamoja na kuweka mazingira rafiki ili kusaidia kupata mikopo inayotolewa na serikali kwa urahisi.

Dodoma tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jiji la dodoma ambapo kwanza nilianza kwa kuwauliza nini kifanyike ili kusaidia vijana wengi kujiingiza katika fursa za uwekezaji hapa Nchini?

Sauti za wananchi

Baadhi ya viongozi wa mitaa akiwemo bw. Alfaksad Ganyara mwenyekiti wa mtaa wa miyuji anatoa wito kwa vijana kuwa na utaratibu wa kutembelea katika ofisi za serikali za mitaa ili kuweza kupata taarifa mbalimbali hususani fursa zinazotolewa na serikali

Sauti ya mwenyekiti.