Dodoma FM

Zaidi ya shilingi millioni 300 kujenga miundombinu ya maji Kigwe

4 July 2023, 4:39 pm

Picha ni viongozi mbalimbali wilayani Bahi wakiwa katika Hafla hiyo. Picha na Bernad Magawa.

Wazawa wametakiwa kupewa kipaumbele zaidi katika miradi mbalimbali inayo anzishwa wialayani humo.

Na Bernad Magawa

Zaidi ya Shilingi million 300 zinatarajiwa kujenga miundombinu ya maji katika kata ya kigwe ili kuwaondolea changamoto ya kukosa maji safi wananchi wa kata hiyo iliyowasumbua kwa miaka mingi huku visima 8 vikitarajiwa kuchimbwa vijiji mbalimbali ndani ya wilaya ya Bahi.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vyeti kama ishara ya kuanza kutekelezwa kwa miradi ya maji, Mgeni wa heshima katika hafla hiyo  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima amewaagiza watumishi wa serikali kuhakikisha wanawasaidia wakandarasi  ili kukamilisha mirad hiyo kwa wakati.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi .
Picha ni viongozi mbalimbali wilayani Bahi wakiwa katika Hafla hiyo. Picha na Bernad Magawa.

Nao viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe Kenneth Nollo pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Mhe. Donald Mejiti (MNEC) wamezungumzia miradi hiyo huku Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Bahi Denis  Komba akielekeza wazawa kupewa kipaumbele katika kazi ndogondogo kwenye miradi hiyo.

Sauti za viongozi.

Awali meneja wa Ruwasa wilaya ya Bahi Robert Mgombela alieleza namna miradi hiyo itakavyotekelezwa huku wakandarasi watakaojenga miradi hiyo wakiishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kutekeleza miradi hiyo kwa wakati nao wananchi wa  kata ya kigwe wakifurahia  kupelekewa maji.

Sauti za wahandisi na wananchi.