Dodoma FM

Wakuu wa Taasisi za Afya watakiwa kuboresha huduma za Afya

12 April 2023, 5:37 pm

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu. Picha na Wizara ya Afya.

Katika Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi, wajumbe watapitia na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwelekeo wa sekta ya afya hususani suala la ubora wa huduma.

Na Pius Jayunga.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo amefungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara na Taasisi zake unaofanyika kwa Siku mbili (Aprili 12-13, 2023) Jijini Dodoma.

Akihutubia katika mkutano huo Waziri Ummy amewataka wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya kuboresha ubora wa huduma za afya ikiwemo lugha nzuri kuanzia mapokezi, muda wanaotumia wagonjwa kupata huduma, upatikanaji wa dawa pamoja na kuimarisha vipimo.

Sauti ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara na Taasisi zake wakiwa katika mkutano huo. Picha na Wizara ya Afya.

Waziri Ummy amewaagiza wakuu wa taasisi zilizopo chini ya wizara ya afya kufanyika maboresho na kutatua changamoto mbalimbali za utoaji huduma za afya katika taasisi zao.

Sauti ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Katika Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi, wajumbe watapitia na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwelekeo wa sekta ya afya hususani suala la ubora wa huduma, miradi ya maendeleo pamoja na kujadili utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 na kuelekea kwenye Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/24.