Dodoma FM

Wazazi, walezi watakiwa kuacha kushinikiza watoto kujifelisha mitihani

23 January 2024, 8:44 pm

Wanafunzi wametakiwa kuachana na vishawishi vya baadhi ya wazazi vya kuwataka kujifelisha pamoja na baadhi ya tamaa za mtaani. Picha na Habari leo.

Hata hivyo changamoto hiyo imekuwa ni kubwa kwa baadhi ya wazazi kuwataka watoto wao kutofanya vizuri katika mitihani yao mwisho.

Na Victor Chigwada
Jamii imetakiwa kuachana na dhana potofu ya kuwakatisha watoto wao masomo kwa kuwawekea shinikio la kujifelisha mitahani yao ya mwisho .

Hii imekuwa desturi kwa baadhi ya wazazi kukosa maono sahihi kwa watoto wao juu ya elimu na badala yake wamekuwa wakiwa ingiza kwenye majukumu yasiyo endana na umri wao.

Baadhi ya wazazi wamesema kuwa watoto wao ni muhimu kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto amabazo zitakuwa msaada kwenye maisha yao na hata familia kwa ujumla.

Sauti za baadhi ya wazazi.

Wameongeza kuwa maisha ya sasa yamekuwa ni magumu kwani vijana wengi wameshindwa kuyamudu hivyo ni vyema Serikali kuwachukulia hatua wazazi wenye tabia hiyo.

Happy John ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza amewasihi wanafunzi wenzake kuachana na vishawishi vya wazazi kuwataka kujifelisha pamoja na baadhi ya tamaa za mtaani.

Sauti ya Mwanafunzi.