Dodoma FM

Uhaba wa maji wahatarisha familia na ndoa za wakazi wa Zepisa

1 November 2023, 10:54 am

Picha ni wakazi wa Kijiji cha Zepisa wakiwa katika foleni ya kusubiri maji kisimani hapo. Picha na Mindi Joseph.

Changamoto ya maji kwa Wakazi wa Zepisa B kata ya  Hombolo Makulu imekuwepo tangu mwaka 1984 Hadi sasa 2023.

Na Mindi Joseph.

Wakazi wa Mtaa wa Zepisa B kata ya Hombolo Makulu Mkoani Dodoma wameomba kutatuliwa changamoto ya maji inayowakabili ili kunusuru Familia na ndoa Zao.

Mtaa wa Zepisa B unawakazi Wapatao 3143 lakini wanatumia kisima kimoja cha maji na kusababisha foleni ya maji huku wanawake wakilazimika kuteka maji usiku wa manane.

Picha ni Wakazi wa kijiji hicho wakizungumzia adha hiyo ya maji .Picha na Mindi Joseph.

Kitendo hicho kimekuwa kikisababisha ndoa nyingi kuvunjika kwa sababu wanawake hulazimika kuamka usiku wa manane na wengine wanalala visimani kama wanavyosimulia.

Sauti za wakazi wa Zepisa.

Mwaka 2001 Mwenyekiti wa Mtaa wa Zepisa B kata ya  Hombolo Makulu Mussa Rashid alifanya jitihada ya kuhakikisha kisima kinachimbwa kijijini hapo.

Sauti ya Bw. Mussa Rashid.