Dodoma FM

Fahamu historia ya kisima cha Bwibwi kilichomeza watu 29

19 May 2023, 6:15 pm

Picha ni Kisima cha kale cha Bwibwi kilichopo eneo la Iyumbu. Picha na George John.

Imani ya watu dhidi ya maji ya kisima hiki ni kubwa, chifu anatueleza na kutuonesha mfano wa kunywa maji haya.

Na Mariam Kasawa.

Bado tunaendelea kukujuza mambo mbalimbali ya kale, historia za kale zinazopatikana mkoani Dodoma kupitia fahari ya Dodoma.

Kamera ya Fahari bado ipo katika himaya ya Bwibwi, safari yetu leo inatupeleka moja kwa moja kwenda kukitazama kisima cha Bwibwi kisima ambacho inasemekana kiligunduliwa na mwindaji miaka mingi iliyopita na baadaye kilitumiwa na watu wa himaya ya chifu Chihoma.

Ukikitazama kisima hiki kwa haraka unaweza ukakiona cha kawaida kwa urefu lakini chifu Lazaro Chihoma anatueleza ukubwa wa kisima hiki .

Chifu Lazaro Chihoma akielekea mahali kilipo Kisima hicho cha Bwibwi.Picha na George John.