Dodoma FM

Serikali yaombwa kuendelea kutoa elimu juu ya kukabiliana na majanga

27 September 2023, 2:34 pm

Picha na Koplo Mery Meso Askari kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji akielezea aina za Majanga.Picha na Katende Kandolo.

Wataalam wamekuwa wakishauri wafanyabiashara, wananchi kufundishwa kukabiliana na majanga ya moto ikiwemo Kuepuka makazi holela, kuhimiza miundombinu ya kisasa pamoja utekelezaji wa sheria upewe kipaumbele.

Katende Kandole.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo ya moto pindi yanapojitokeza.

Ni muendelezo wa kutoa elimu kwa jamii juu ya kupambana na majanga mbalimbali katika jamii ambapo leo Dodoma tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma kuhusiana na uelewa wao kuhusu namna ya kukabiliana na moto.

Je wananzungumziaja juu ya suala hilo?

Sauti za baadhi ya wananchi.
Picha ni gari ya maalum inayotumika katika majanga ya moto kuzima moto. Picha na Katende Kandolo.

Jeshi la zimamoto na uokoaji ni taasisi yenye dhamana ya kutoa elimu kwa jamii juu ya mapambano dhidi ya majanga mbalimbali Koplo Mery Meso Askari kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji leo anaendelea kutujuza mengi juu ya suala hilo.

Sauti ya Koplo Mery Meso.