Dodoma FM

Vijana wazungumzia changamoto za mikopo halmashauri

30 March 2023, 6:14 pm

Vijana hao wamesema kuwa kumekuwa na changamoto na usumbufu mkubwa kwani wanatumia muda mwingi kufuatilia fedha hizo.

Na Victor Chigwada .   

Baadhi  ya vijana wa  kutoka Wilaya ya Chamwino wamezungumzia changamoto wanazozipata katika Halmashauri  pindi wanapoenda kuchukua mikopo inayotengwa na serikali kwaajili yao

Aidha wameiomba Serikali kuongeza fungu la fedha katika Halimashauri nchini ili wapate fedha hizo sawa na mahitaji yao .

 Joseph Mpilimi  ni mwenyekiti wa kijiji cha Mlebe amekiri kuwa kumekuwa na changamoto  katika kupata mikopo inayotengwa na serikali kupitia Halmashauri hali inayokatisha tamaa vijana

Naye Afisa maendeleo ya jamii wa Kata ya Msamaro Bi.Ng’washi Mhuli amesema kuwa  bajeti za Halmashauri zimekuwa zikichangia   vikundi kushindwa kutimiza malengo yao

Mhuli ameomba mashirika mbalimbali  kuwasaiidia vijana kimawazo na hata kuwawezesha kifedha ili kuwanufaisha katika shughuli za vikundi  vyao

Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kujiajili na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kwa kutoa mikopo isiyo na riba.