Dodoma FM

Wakulima wilayani Kondoa washauriwa kuhifadhi mazao yao kwa njia ya asili na kisasa ili kuepuka sumu kuvu

13 August 2021, 12:24 pm

Na; Benard Filbert.

Ikiwa ni wakati wa mavuno wakulima katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma wameshauriwa kuhifadhi mazao yao kwa njia za asili na kitaalamu ili kuepuka kupatwa na sumu kuvu ambayo ni hatari kiafya.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa idara ya kilimo na ushirika Wilaya ya Kondoa Bw. Hassan Kiseto wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema kuna njia ya asili pamoja na ya kitaalamu ambazo zimekuwa zikikubalika katika uhifadhi wa mazao.

Amesema kwa wale wanaotumia sumu kuhifadhia mazao hawatakiwi kutumia mazao hayo bila kuoshwa kutokana na kuwa na uwezekano wa madhara kiafya.

Hata hivyo amesema wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kwa wakulima ili waangalie namna bora ya kuhifadhi mazao hususani katika mikutano ya hadhara kupitia kwa maafisa kilimo wa Kata.

Wakulima Nchini wanashauriwa kuangalia njia bora za kuhifadhi mazao ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.