Dodoma FM

Jamii imetakiwa kuzingatia njia za kujikinga na ugonjwa wa malaria msimu wa masika

4 November 2021, 12:19 pm

Na;Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa jamii kuzingatia njia za kujikinga na ugonjwa wa malaria katika kipindi hiki cha masika.

Akizungumza na Taswira ya habari Dr. Chesco Muhema kutoka hospitali ya mkoa wa Dodoma amesema kuwa wakati mvua ni hatari kwa mbu wa enezao ugonjwa huo kuzaliana, hivyo jamii izingatie usafi wa mazingira ili kuepukana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa kwa mkoa wa Dodoma ugonjwa wa malaria unapotea kutokana na juhudi mbalimbali za serikali zilizofanyika ikiambatana na ugawaji vyandarua vyenye dawa ,hivyo elimu inahitajika zaidi kwani kuna baadhi ya maeneo ugonjwa huo unaathiri na kusababisha vifo vya kina mama na watoto.

Kwa upande wao vijana jijini hapa wamesema kuwa kuna haja ya wao kuikumbusha jamii juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Tanzania imepiga hatua kubwa katika juhudi za kuzuia na kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kuhimiza matumizi ya vyandarua vyenye dawa.