Dodoma FM

DUWASA yaendelea kutekeleza azma ya kuifanya Dodoma ya kijani

18 March 2024, 5:34 pm

Picha ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shekimweri akiongea katika zoezi hilo la upandaji miti. Picha na Seleman Kodima.

Utekelezaji wa zoezi hilo unabeba dhana ya kuhakikisha maeneo ya vyanzo vya maji yanakuwa salama katika athari za mabadiliko ya tabianchi.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri  ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kukijanisha Dodoma kwa upandaji wa miti katika eneo la Tanki kubwa la maji Nzuguni.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa zoezi la upandaji wa miti 300 kwenye eneo la Tanki kikubwa la maji linalopatikana Nzuguni.

Alhaji Jabiri Shekimweri amesema kuwa kitendo cha mamlaka hiyo kutii agizo lake la kupanda miti yenye kimo cha wastani kitawezesha miti hiyo kukua bila changamoto yeyote ya kimazingira.

Sauti ya Mh. Jabir Shekimweri.
Picha ni Tanki kubwa la maji lililopo Nzuguni Jijini Dodoma . Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa kuanzia Novemba mwaka jana hadi leo jumla ya miti 2000 imepandwa katika maeneo tofauti ya vyanzo vya maji ikiwa ni utekelezaji na utunzaji wa vyanzo hivyo.

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph .