Vijana wageukia kilimo kupambana na ukosefu wa ajira
29 May 2026, 18:03

kilimo si kazi ya watu masikini ni fursa ya kutoka kimaisha.
Na Victor Chigwada.
Vijana walio hitimu masomo Yao katika vyuo mbalimbali wamejikuta wakibobea katika shughuli za kilimo Ili kuendesha maisha yao.
Wakiongea na Taswira ya habari baadhi ya vijana wamesema kuwa wamejikita katika shughuli za kilimo kutokana na changamoto ya uhaba wa ajira nchini hali ambayo imebadilisha ndoto zao za taaluma .
Taswira ya habari ilizungumza na Afisa maendeleo wa kata ya msamalo Bi.Ngw’ashi Muhuri ambapo aliwapongeza vijana wanao chukua hatua za kuwekeza kwenye shughuli ya kilimo amewataka vijana hao kutambua kuwa kilimo si kazi ya watu masikini ni fursa ya kutoka kimaisha.
Pia amewataka vijana hao wanao jishulisha na kilimo kujikita katika kilimo chenye tija ili waweze kunufaika na kazi hiyo.