Dodoma FM

Matumizi ya visikizi kwa muda mrefu hatari kwa usikivu

14 August 2026, 16:16

Matumizi ya visikizi/ vipokea sauti vinaweza kuwa na madhara kwa matumizi visipotumiwa vizuri. Picha na mtanda.

Wataalamu wanashauri watumiaji wa earphones kupunguza kiwango cha sauti, kuepuka kuzitumia kwa muda mrefu bila mapumziko na kuzingatia afya ya masikio ili kujilinda dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza baadaye.

Na Grace Budodi.                                             

Matumizi ya earphones (kifaa cha kusikilizia sauti) kwa muda mrefu miongoni mwa vijana yamekuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku, huku baadhi wakizitumia kusikiliza muziki, kusikiliza sauti ya    video na hata kupunguza mawazo wanapokuwa wapweke.

Kwa baadhi ya vijana, earphones si kifaa cha kusikiliza muziki pekee, bali pia ni njia ya kujiburudisha, kupunguza mawazo na kujitenga na mazingira yanayowazunguka.

Jijini Dodoma, baadhi ya vijana wanasema hutumia earphones kwa muda mrefu, hasa wanapokuwa hawana shughuli za kufanya.

Ingawa matumizi hayo yamekuwa sehemu ya kawaida ya maisha yao, wataalamu wa afya wanaonya kuwa muda ambao mtu hutumia earphones pamoja na kiwango cha sauti anachosikiliza vinaweza kuamua iwapo matumizi hayo yatakuwa salama au la.

Daktari Jeffta Fabiani wa Hospitali ya Benjamin Mkapa anasema matumizi ya earphones kwa muda mrefu, hususan kwa sauti kubwa, yanaweza kuanza kuathiri uwezo wa kusikia na hatimaye kusababisha mtu kupoteza kabisa uwezo huo.

Mbali na uwezo wa kusikia, Daktari Fabiani anaeleza kuwa masikio vina jukumu muhimu katika kusaidia mwili kudumisha uwiano wakati wa kusimama na kutembea, hivyo matatizo yanayohusisha masikio yanaweza pia kumuathiri mtu katika hali ya usikivu.

Sauti na Grace Budodi.