Dodoma FM

Wizara ya afya yasisitizi wa umuhimu wa elimu ya afya ya akili

4 September 2026, 16:02

Ni muhimu kuendelea kuwaimarisha wataalamu wa afya ili waweze kutoa huduma bora kwa watu wenye changamoto za afya ya akili. Picha na mtandao.

Mafunzo hayo yanayofanyika jijini Dodoma ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma kwa watu wenye changamoto ya matumizi ya pombe, huku wadau wakisisitiza umuhimu wa kuunganisha huduma za afya ya akili na huduma nyingine za afya nchini.

Na Elizabeth Mwinuka.                                                                                       

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, amesisitiza umuhimu wa kuipa kipaumbele afya ya akili nchini, akieleza kuwa ni sehemu muhimu ya afya ya mtu na inahitaji kupewa uzito katika mipango na utekelezaji wa huduma za afya

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Usimamizi wa Tatizo la Matumizi ya Pombe kwa kutumia dawa ya Naltrexone, yanayolenga kuongeza uwezo wa wataalamu katika kukabiliana na changamoto za matumizi ya pombe

Amesema ni muhimu kuendelea kuwaimarisha wataalamu wa afya ili waweze kutoa huduma bora kwa watu wenye changamoto za afya ya akili, pamoja na kuhakikisha elimu na maarifa kuhusu afya ya akili yanafika katika familia na jamii.

Sauti na Elizabeth Mwinuka.