Wananchi waomba kutengewa maeneo ya wazi kwaajili ya mazoezi
19 August 2026, 16:34

Uhaba wa viwanja pamoja na miundombinu rafiki kwa michezo unawafanya vijana kukosa maeneo maalum ya kufanya mazoezi na kukuza vipaji vyao.
Na Ramadhani Juma.
Baadhi ya wananchi jijini dodoma wameiomba serikali kuongeza na kuboresha viwanja vya michezo na maeneo maalum ya mazoezi ili kuwawezesha vijana kuendeleza vipaji vyao na kushiriki michezo kwa uhuru.
Wananchi hao wamesema uhaba wa viwanja pamoja na miundombinu rafiki kwa michezo unawafanya vijana kukosa maeneo maalum ya kufanya mazoezi na kukuza vipaji vyao, huku baadhi ya michezo ikikosa nafasi ya kutosha katika maeneo ya makazi.
Afisa michezo jiji la Dodoma Bi. Neema Kilongola ameeleza kuwa viwanja vya wazi kwaajili ya mazoezi na michezo vipo ila wananchi wamekuwa wakivamia maeneo hayo na kufanya shughuli zingine .
Ikumbukwe kuwa mnamo January 29 , 2026 Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba alizitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha maeneo ya wazi yaliyopo katika mitaa na kata mbalimbali hayauzwi, bali yaachwe kwa ajili ya mazoezi na shughuli za