Dodoma FM

Wananchi zaidi ya laki moja kunufaika na mradi wa maji Mbulu

18 July 2025, 4:31 pm

Picha ni mradi huo wa maji ambao unagharimu Shilingi bilioni 41.2.Picha na Kitana Hamis.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, ameeleza kuridhishwa na namna RUWASA inavyosimamia utekelezaji wa mradi huo.

Na Kitana Hamis.
Jumla ya wananchi 133,737 kutoka viji 21 vya Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia Mradi wa Maji wa Dambia-Haydom unaoendelea kutekelezwa wilayani humo.

Akizungumza wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipokagua mradi huo, Meneja wa wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijjini (RUWASA) Wilaya ya Mbulu, Mhandisi Onesmo Mwakasege, alisema mradi huo mkubwa unalenga kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa vijiji 21 wilayani humo.

Kwa mujibu wa Mwakasege, ujenzi wa mradi huo unagharimu Shilingi bilioni 41.2 na unatekelezwa na mkandarasi Kings Building kutoka ijini Dar es Salaam.

Habari kamili