Dodoma FM
Dodoma FM
3 March 2026, 15:31

Huduma zingine ni za tiba ya maumivu, huduma ya upasuaji rekebishi wa viungo vilivyopooza, huduma ya upasuaji wa uvimbe na ubongo kwa kutumia teknolojia ya fluorescein na kuanza kwa wodi mpya za kisasa za ‘premier’ kwa ajili ya wagonjwa maalum na wakimataifa ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa maalum na wakimataifa.
Na Benard Filbert.
Katika kipindi cha mwaka 2025 Taasisi ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) imefanikiwa kuhudumia wagonjwa laki moja na elfu themanini (180,000) huku kati yao elfu kumi (10000) wakipewa huduma za kibobezi kutokana na matatizo ya mifupa,ubongo,uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu.
Hayo yemeelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya katika mkutano na Waandishi wa Habari, jijini Dodoma – Machi 2, 2026
Amesema moja ya mfanikio makubwa ambayo taasisi hiyo imepata ni kuweza kuhudumia Kundi kubwa la watu ikilinganishwa na hapo awali.
Aidha amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuongeza huduma mpya 9 ambazo hapo awali hazikuwepo huku huduma hizo ikiwa ni pamoja na matumizi ya akili unde katika huduma za upasuaji ikitoa msaada mkubwa kwa wataalamu ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Kadhalika amesema kuanzishwa kwa huduma hizo kumerahisisha kuhudumia wagonjwa wengi kwa muda mfupi na kupunguza malalamiko ya wagonjwa kutokuhudumiwa.
Taasisi ya mifupa na ubongo muhimbili (MOI) ni taasisi ya kitaifa ya matibabu ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu (neurosurgery) iliyopo Dar es Salaam, Tanzania, ndani ya eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbilih uku majukumu yake ikiwa ni huduma za kibingwa Matibabu ya mifupa, majeraha (trauma), upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo Rufaa ya kitaifa Inapokea wagonjwa wa rufaa kutoka hospitali za mikoa yote Tanzania na wakati mwingine nchi jirani.