Dodoma FM

Wananchi Handali wapongeza ukarabati matundu ya vyoo katika zahanati

29 July 2026, 15:56

Wamesema hapo awali mazingira ya vyoo katika kituo hicho cha afya hayakuwa mazuri.Picha na Mtandao.

Hapo awali mazingira ya vyoo katika kituo hicho cha afya hayakuwa mazuri na salama kwa afya za watumiaji.

Na Victor Chigwada.

Ukarabati na ujenzi wa matundu ya vyoo katika kituo Cha afya Handali umeleta ahueni kwa wananchi wanao fika kituoni hapo kupata huduma za matibabu.

Wamesema hapo awali mazingira ya vyoo katika kituo hicho cha afya hayakuwa mazuri na salama kwa afya za watumiaji kupitia ukarabati uliofanyika utaongeza usalama kwa wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.

Nae mjumbe wa bodi ya kituo hicho cha afya Bw.Mashauri Machea amekiri kuwepo Kwa ujenzi wa matundu ya vyoo bora na pia baadhi ya matundu yanatengezwa maalum kwaajili ya watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kichomea taka.

Kwasasa ujenzi huo upo katika hatua za mwisho kabla ya kukabidhiwa na kuanza kutumika rasmi.

Sauti ya Victor kina.

Naye Emmanuel Madali Diwani wa Kata ya Handali amekiri kuwepo kwa ujenzi huo katika kituo Cha afya huku wakiendelea kushughulikia  mapungufu mengine yaliyopo katika kituo hicho.