Dodoma FM

Bodaboda waeleza sababu za kushindwa kumaliza mikataba kwa wakati

17 September 2026, 12:14

Picha ni maafisa usafirishaji almaarufu kama bodaboda katika moja ya kijiwe katika kata ya Majengo jijini Dodoma.Picha na Dodoma fm.

Hata hivyo, waajiri wanashauri kuwepo kwa mfumo wa wazi wa kupima utendaji wa maafisa usafirishaji, kuweka malengo yanayotekelezeka na kutoa mrejesho wa mara kwa mara ili changamoto zinapojitokeza ziweze kutatuliwa kabla ya kumalizika kwa mkataba.

Na Mathias Mgale.

Kushindwa kwa baadhi ya maafisa usafirishaji kumaliza mikataba yao ya kazi kwa wakati kumehusishwa na sababu mbalimbali ikiwemo kutokidhi vigezo vya utendaji, changamoto za kiutendaji pamoja na kutofikia malengo yaliyowekwa katika kipindi cha mkataba.

Baadhi ya wadau wa  usafirishaji wameeleza kuwa, pamoja na kuwa mkataba una muda maalum, utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi unahitaji afisa kuwa na mipango mizuri ya kazi, nidhamu, uwajibikaji na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumzia changamoto zinazoweza kuwafanya baadhi ya maafisa usafirishaji kushindwa kukamilisha mikataba yao kwa wakati, Anselimo Paul  ambaye ni afisa usafirishaji anayetoa mikataba kwa vijana amesema baadhi ya sababu ni pamoja na vijana wengi kupenda starehe na kuwa na matumizi mabaya ya fedha.

Ripoti ya Mathias Mgale.