Wachimbaji wa dhahabu handali walalamika kukosa bei elekezi
9 July 2026, 16:37

Serikali kupitia Wizara ya Madini inaendelea kusogeza huduma karibu na wananchi Kwa kuanzisha masoko 44 na vituo vidogo 120 vya ununuzi wa dhahabu nchi nzima masoko haya yatatoa bei elekezi na yanalenga kuondoa udanganyifu Kwa wachimbaji .
Na Victor Chigwada.
Wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Handali wamelalamikia kukosa bei elekezi ya mauzo ya dahabu na kujikuta wakiuza kwa bei ya hasara.
Wachimbaji hao wameiomba serikali kuwaletea soko la uhakika la uuzaji wa dhahabu ili iwasaidi kujipatia kipato na kukuza uchumi wa kijiji hicho.
Aidha wachimbaji hao wamedai kuwa licha ya kazi ngumu wanayo ifanya wanunuzi wa dhahabu wanao fika kununua dhahabu wamekuwa wakijipangia bei wenyewe na kujikuta wakiuza kwa bei ya hasara.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Handali Mashauli Machea amekiri kuwa ukosefu wa elimu ya biashara wa jinsi ya kuuza dhahabu hiyo unapelekea wachimbaji hao kuuza kiholela dhahabu kwa walanguzi .
Machea ameongeza kuwa wachimbaji wadogo wadogo wa eneo hilo wanakabiliwa na ukosefu wa elimu ya uchumbaji na mauzo licha ya kuwa na leseni za uchimbaji .