Dodoma FM

Serikali yaendelea kuchukua tahadhari kudhibiti Polio Nchini

12 September 2023, 12:26 pm

Picha ni waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika mkutano na waandishi wa habari.Picha na Yussuph Hassan.

Aidha wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Viongozi mbalimbali wametakiwa kusimamia Kampeni ya Kitaifa ya chanjo ya matone pamoja na Waganga wa Mikoa kutoa chanjo hiyo kwa wakati sambamba na kutoa elimu kwa jamii.

Na Yussuph Hassan.

Serikali imeendelea kuchukuwa tahadhari mbalimbali ili kuzia ugonjwa wa polio usiingie Nchini.

Waziri wa Afya Ummy Mwalim, amesema katika kuhakikisha Tanzania inadhibiti ugonjwa wa polio, hivi karibuni itaendesha kampeni ya chanjo ya matone katika Mikoa sita Nchini.

Sauti ya Waziri Ummy Mwalimu.
Picha ni baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo picha na Yussuph Hassan.

Aidha Waziri Ummy amefafanua tofauti ya chanjo hii na chanjo nyingine za ugonjwa polio kufuatia kupatikana kwa Mgonjwa mwingine wa polio tangu Mwaka 1996.

Sauti ya Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy pia ameainisha takwimu za watoto ambao hawajapata chanjo yoyote na wale waliopata chanjo moja.

Sauti ya Waziri Ummy Mwalimu.