Dodoma FM

Serikali yapongeza ujenzi wa shule ya sekondari lenjulu kongwa

26 April 2023, 1:52 pm

Mh Ndejembi akisalimiana na viongozi wa kata ya Lenjulu . Picha na Benadetha Mwakilabi.

Amewataka wakazi wa Lenjulu kutunza miundombinu na mazingira ya shule hiyo na kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule na kusoma kwa bidii.

NA Bernadetha Mwakilabi.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Deogratias Ndejembi amepongeza uongozi wa wilaya ya Kongwa kwa ujenzi wa shule ya sekondari Lenjulu iliyopo kata ya Lenjulu wilayani humo kwa kuwa ya kwanza nchi nzima ambayo miundombinu yake imekamilika kwa bajeti iliyopangwa.

Ndejembi ameyasema hayo katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule hiyo iliyojengwa kupitia mradi wa SEQUIP na kugharimu shilingi milioni 470, ambapo ameahidi pia kutatua suala la maji shuleni hapo.

Sauti ya Mh. Deogratias Ndejembi

Aidha Ndejembi amewataka wananchi wa Lenjulu kutunza mazingira na miundombinu ya shule hiyo na kuhakikisha watoto wanaenda shule na kusoma ili jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ziweze kuzaa matunda.

Sauti ya Mh.Deogratias Ndejembi
Katika ziara hiyo Pia waziri Ndejembi alipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi wa sekondari ya Lenjulu. Picha na Benadetha Mwakilabi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lenjulu Mheshimiwa Briton Chisongela ameomba serikali kuongeza idadi ya walimu shuleni hapo ili kuwasaidia wanafunzi kufaulu vizuri.

Sauti ya Diwani wa kata ya Lenjulu.

Akijibu hoja ya upungufu wa walimu Ndejembi amesema kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi kupitia mchakato wa ajira za walimu uliotangazwa hivi karibuni.

Sauti ya mh. Ndejembi