Dodoma FM

Majukumu ya Nyumbani yarudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike

25 January 2023, 4:26 am

Na; Mariam Matundu.

Majukumu mengi ya kazi za nyumbani kwa watoto wa kike imetajwa kuwa ni moja ya sababu inayorudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa wasichana .

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa mtaa wa Hombolo bwawani jana katika siku ya kimataifa ya elimu na kusema kuwa ni muhimu wazazi kuweka mgawanyo sawa wa majukumu kwa wasichana na wavulana .

Mwenyekiti wa mashujaa wa maendeleo kata ya Hombolo Abel Nyamliga amesema pia ni muhimu wazazi kuweka urafiki na watoto wao ili kuwafanya kuwa huru kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo ukatili ambao pia unakwamisha wasichana kupata elimu.

Mariam Matundu anayo taarifa zaidi.