Dodoma FM

Uongozi wa kata ya Itiso yatoa pongezi kwa jitihada za ujenzi wa madarasa

9 March 2023, 4:35 pm

Ujenzi wa Vyumba vya madarasa kata ya Itiso wilayani Chamwino .Picha na Swahili news

Uongozi umetoa pongezi kwa wananchi wa kata ya Itiso wilayani Chamwino kwa juhudi kubwa wanayoifanya ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa .

Na Victor Chigwada.

Uongozi wa Kata ya Itiso wilayani Chamwino umetoa pongezi kwa wananchi wa kata hiyo kwa juhudi kubwa wanayoifanya ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa .

Pongezi hizo zimetolewa na Diwani wa kata hiyo Simoni Mtambila wakati akizungumza hatua inayofanyika ndani ya kata hiyo kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kupitia nguvu za wananchi

Matambila amesema kuwa licha ya kuwa na mapungufu ya vyumba vya madarasa lakini nguvu za wananchi zimeendela kutumika katika shule za vijiji ili kupunguza adha hiyo.

Sauti ya Diwani Simoni Mtambila.

Ameongeza kuwa ni vyema Serikali kuongeza nguvu ya uwekezaji upande wa elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza idadi ya walimu shuleni.

Sauti ya Diwani Simoni Mtambila.

Aidha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shikombo Kata ya Itiso wameiomba Serikali kuunga mkono juhudi zao katika upande wa elimu kwa kuwasaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuongeza idadi ya walimu.

Sauti za wananchi