Dodoma FM

Wilaya ya Bahi yaagizwa kuongeza shule za kidato cha nne na tano

10 July 2023, 2:56 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi (MNEC) Donald Mejitii akizungumza wakati wa Baraza la madiwani.Picha na Bernad Magawa.

Mheshimiwa Godwin Gongwe ameahidi kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa Maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa.

Na Bernad Magawa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Sitaki Senyamule ameuagiza uongozi wa wilaya ya Bahi kuongeza shule za kidao cha tano na sita ili watoto wanaofaulu kidato cha nne wilayani humo wapate nafasi za kuendelea na masomo baada ya wilaya hiyo yenye tarafa nne kuwa na shule moja tu ya kidato cha tano na sita.

Senyamule ameyasema hayo wakati akizungumza na Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bahi alipotembelea wilayani humo na kuelekeza viongozi huhamasisha wananchi kuanza ujenzi wa maboma ili serikali iunge mkono kwa kumalizia majengo huku akiwaagiza  Madiwani kuhakikisha wanawakumbusha wananchi wao kutunza chakula ili kuepuka uwepo wa njaa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Senyamule akiwasili halmashauri ya wilaya ya Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Mkuu huyo wa Mkoa amewahimiza waheshimiwa Madiwani kuendelea kuwahamashisha wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo inayopelekwa na serikali wilayani Bahi ili kuunga mkoni juhudi za serikali.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mheshimiwa Donard Mejitii alimkaribisha Mkuu wa mkoa kuzungumza na Madiwani huku Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mheshimiwa Godwin Gongwe akiahidi kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa Maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi na Mkuu wa wilaya ya Bahi.