Dodoma FM

kujengwa kwa soko la kimataifa Kongwa kutaongeza fursa za ajira

17 May 2021, 1:22 pm

Na; Benard Filbert

Kujengwa kwa chuo cha kilimo pamoja na soko la mazao la kimataifa katika Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa imeelezwa itaongeza fursa nyingi za ajira kwa wananchi wa eneo hilo.

Hayo yameelezwa na diwani wa Kata hiyo Bw.Joel Shedrack Musa  wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utekelezaji wa mradi huo.

Bw.Joel amesema chuo hicho kinafadhiliwa na shirika la chakula Duniani WFP ambapo amewataka wakazi wa Kata hiyo kuchangamkia fursa hizo mara baada ya kuanza kwa mradi huo ili ziwasaidie kuinuka kiuchumi.       

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mtanana wamesema wapo tayari kuchangamkia fursa hiyo pindi ujenzi wa mradi huo utakapoanza.

Mradi wa ujenzi wa chuo cha kilimo na soko la mazao pamoja na mashine za kusindika unga unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu katika Kata ya Mtanana huku ukifadhiliwa na shirika la chakula Duniani WFP huku ukikadiriwa kutumia shilingi bilion 16 za kitanzania.