Dodoma FM

Wazazi: Vijana wageuze elimu zao kuwa chanzo cha ajira

18 May 2021, 7:41 am

Na; Alfredy Sanga

Baadhi ya vijana wameeleza jinsi ambavyo kijana anaweza kujiajiri na kutafuta fursa mbali mbali katika kujikwamua kimaisha, badala ya kutegemea kuajiriwa  kutokana na ukosefu wa ajira nchini.

Wakizungumza na taswira ya habari vijana hao wamesema kitu kikubwa kwa kijana anaye jiajiri ni pamoja na kuzingatia ubunifu ambao utamtofautisha na mtu mwingine.

Wamesema pia kutochagua kazi ni moja ya sababu inayoweza kumsaidia kijana kwani mtaani kuna vibarua na kazi ndogondogo za kujiingizia kipato.

Nao baadhi ya wazazi  wamewahimiza vijana kugeuza elimu zao kuwa chanzo cha ajira badala ya kutumia muda mwingi mtandaoni kufatilia vitu vingi ambavyo havina manufaa katika maisha yao.

Naye  mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) , Ndg, Geodfrey Casemilo, amesema changamoto kubwa ya vijana kujiajiri ni mtaji huku akibainisha kuwa kuwa kujenga mahusiano mazuri na jamii kunaweza kuwafungulia fursa mbalimbali za ajira.