Dodoma FM

Wananchi watakiwa kushiriki wiki ya ufuatiliaji na tathmini

28 August 2023, 3:22 pm

Mtakwimu Mkuu kutoka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Ofisi Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Bw. Thomas Saguda, alipokuwa akizungumza na katika kipindi cha #Themorningpowershow. Picha na DMG Digital.

Kongamano hili la Pili la Kitaifa la Wiki yaUfuatiliaji na Tathmini litakalofanyika Jijini Arusha mapema mwezi Septemba, itawalenga zaidi,wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini,Maafisa na Mameneja wa Miradi kutoka katika Taasisi zote za Umma,Taasisi Binafsi, makampuni, Asasi za Kiraia na mashirika ya Kimataifa.

Na Alfred Bulahya.

Wananchi wamepewa wito wa kushiriki katika wiki ya Kitaifa yaUfuatiliaji na Tathmini itakayofanyika Jijini Arusha ambayo itahusishakutoa elimu itakayowawezesha kutoa taarifa za Ufuatiliaji na Tathminina Ufuatiliaji wa Miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayofanywa naSerikali katika maeneo yao.

Hayo yameelezwa leo Tarehe 28 Agosti 2023, na Mtakwimu Mkuu kutokaIdara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Ofisi Waziri Mkuu (Sera, Bunge naUratibu) Bw. Thomas Saguda, alipokuwa akizungumza na katika kipindi cha #Themorningpowershow kinachorushwa na @dodoma_tvBwn. Saguda Alisema, Wananchi hao wanaweza kushirki kupitia maoneshombalimbali yatakayoonesha kazi mbalimbali za Ufuatiliaji na Tathminizilizofanyika ndani ya nchi na kupata kujionea mengine yatayooneshwana washiriki mbalimbali kutoka nje ya nchi.

“Maonesho haya yatawapa fursa wananchi ya kuelewa namna wanavyopaswakufanya Ufuatiliajia na Tathmini, wenzetu wataalam wanaita CitizenScience, ni rahisi sana Mwananchi ukimuuliza mradi flani wa maji paleumefanya kazi, atakwambia unafanya kazi, ama atakwambia maji paleyalitoka wiki mbili tuu yakakatika, kwa hiyo yule anakupa taarifa yauhakika, kwa sababu ndiyo mnufaika na ndiyo mlengwa.” Alisema bwanaSaguda.

Amesema kuwa Sambamba na Maonesho hayo Kongamano hilo pialitahusisha mafunzo ya kitaaluma, warsha mbalimbali zitakazoendeshwana wataalamu wabobezi wa masuala ya Ufuatiliajia na Tathmini kutokandani na nje ya nchi na kuongeza kusema kuwa mada mbali mbalizimekwisha wasilishwa kwa ajili ya Utekelezaji.

Mtakwimu Mkuu kutokaIdara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Ofisi Waziri Mkuu (Sera, Bunge naUratibu) Bw. Thomas Saguda, alipokuwa akizungumza na katika kipindi cha #Themorningpowershow kinachorushwa na @dodoma_tv.Picha na DMG Digital.

Awali akiongea katika kipindi hicho maalum, Mkurugenzi Msaidizi wIdara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Bw. JohnBosco Quman, alisema Eneo la Ufuatiliaji  naTathmini linamgusa kila mmoja, aliyepo Serikalini au katika Sekta

Binafsi kwani Utekelezaji wa Miradi mingi inatekelezeka katika jamiina inamgusa kila mmoja, “Ukiangalia katika ngazi ya Wizara Sera ndo zinatekelezeka huko, lakini kwenye suala la utekelezaji linashuka

kwenye ngazi ya Halmashauri na ndiko kwenye wadau mbalimbali, kwahivyo kwa kupitia miradi kama vile ya Afya na Maji, Serikali inavyotoafedha na kusimamia miradi hiyo, matokeo yake yanamgusa kila mmoja.”Alibainisha Bw.

Quman Aliendelea Kufafanua kuwa Idara hii ina jumuku kubwa la kuhakikishakuwa kile ambacho kinachotolewa na Serikali kinaenda kunufaisha  jamiinzima.