Dodoma FM

Mgogoro wa ardhi Mpamaa wapelekea nyumba 15 kubomolewa

16 July 2026, 16:28

Baadhi ya waathirika wamesema wameishi eneo hilo kwa muda mrefu na hawaijui taasisi ya Imamu Taqwa.Picha na Noah Patrick.

Zaidi ya nyumba 15 zimebomolewa katika eneo hilo, huku familia kadhaa zikibaki bila makazi na mali zao kuharibika.

Na Bennard Filbert.

Wakazi wa Mtaa wa Mpamaa Block 7, Kata yaMiyuji jijini Dodoma wamelalamikia kubomolewa nyumba zao kufuatia mgogoro wa ardhi unaodaiwa kuanza mwaka  2016.

Wakizungumza na Dodoma FM, baadhi ya waathirika wamesema wameishi eneo hilo kwa muda mrefu na hawaijui taasisi ya Imamu Taqwa inayodaiwa kumiliki ardhi hiyo.

Wamedai kuwa mgogoro huo uliwahi kufikishwa mahakamani na baadaye kurejeshwa Baraza la Ardhi la Kata, ambako walishinda shauri hilo, lakini hawafahamu kilicho sababisha nyumba zao kubomolewa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Imamu Taqwa Yussuph Hussein Saibu amekiri taasisi hiyo kuhusika na ubomoaji huo, akisema ulifanyika kwa kutekeleza amri ya Mahakama ya Rufani baada ya kushinda kesi ya umiliki wa eneo hilo.

Sauti ya Yussuph Hussein Saibu.