Dodoma FM

Bei ya sare na vifaa vya shule yapaa

4 January 2024, 4:42 pm

Picha ni Sare za shule katika soko la Machinga complex Jijini Dodoma zikiwa zimepangwa kwaajili ya kuuzwa kwa wateja.Picha na Thadei Tesha.

katika soko la machinga complex bidhaa zinazoonekana kushamiri ni pamoja na sare za shule kama mashati, sweta za shule madaftari pamoja na viatu vya shule.

Na Thadei Tesha.
Wakati wanafunzi wakijiandaa kufungua shule kwa ajili ya kuanza masomo yao kwa mwezi januari bei za vifaa vya shule ikiwemo sare na vifaa vya kusomea imeendelea kupanda maradufu.

Hili ni soko la machinga complex lililopo jijini Dodoma ambapo kwa sasa shughuli ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali inaendelea hapa huku sare za shule na vifaa vya kujifunzia vikionekana kwa wingi.
Baadhi ya wanunuzi wa bidhaa hii wanasema kwa sasa bei za Sare ya shule pamoja na vifaa vya kujifunzia imepanda kwa kiasi kikubwa.

Sauti za baadhi ya Wanunuzi.
Picha ni vifaa vya shule katika soko la Machinga complex Jijini Dodoma zikiwa zimepangwa kwaajili ya kuuzwa kwa wateja.Picha na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wanaeleza sababu inayochangia bei za sare ya shule na vifaa vya kujifunzia kuwa juu miongoni mwa sababu zinazotajwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya wauzaji kutumia kama fursa ya kupata faida..

Sauti za Baadhi ya Wafanyabiashara.