Dodoma FM

Kamati za shule zatakiwa kuwashirikisha wazazi kuleta mabadiliko

28 June 2023, 5:09 pm

Baadhi ya wajumbe wa kamati za shule kutoka kata nne za wilaya ya Chamwino wakiwa katika mafunzo hayo. Picha na Seleman Kodima.

Ahadi hiyo wameitoa  wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya uwajibikaji na ufatiliaji kwa jamii yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la AFNET kuanzia 27-28 Juni jijini Dodoma.

Na Seleman Kodima.

Wajumbe wa kamati za shule katika kata nne wilayani Chamwino mkoani Dodoma wameahidi kuleta mabadiliko ndani ya kamati hizo ili kufanikisha lengo la utoaji wa elimu bora shuleni.

Baadhi ya wajumbe wa kamati za shule  wakizungumza na Taswira ya Habari wamesema kupitia mafunzo hayo yawe chachu kwa kwenda kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii hususani utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Sauti za baadhi ya wajumbe.
Baadhi ya wajumbe wa kamati za shule kutoka kata nne za wilaya ya Chamwino wakiwa katika mafunzo hayo. Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET Bi. Joy Njelango ambaye amefunga mafunzo hayo,  amesema kupitia semina hiyo wanataraji kuona wajumbe wa kamati za shule wakiwashirikisha wazazi katika masuala mbalimbali yanayohitajika katika utatuzi na utekelezaji wa utoaji wa elimu bora shuleni.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET.

Nae mwenyekiti wa mafunzo hayo amesema yapo mambo ambayo wajumbe walikuwa hawafahamu mipaka ya kazi zao ndani ya kamati ya shule hivyo kupitia mafunzo hayo wamepata dira ya wapi wanatakiwa kwenda kufanya kazi .

Sauti ya Mwenyekiti wa mafunzo hayo.