Dodoma FM

Ubovu wa miundombinu wachangia nauli kupanda Engusero

5 February 2021, 1:47 pm

Na,Seleman Kodima,

Dodoma.

Ubovu wa miundombinu ya barabara katika Kata ya Engusero Wilayani Kiteto umewatia hofu wananchi kuhusu kupata huduma za kijamii wakati huu wa Msimu wa Mvua za Masika.

Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wanakijiji wa Kata hiyo wamesema wamekuwa wakipata shida kufika katika maeneo ya huduma za kijamii, hali inayochangiwa na hali ya miundombinu ya barabara.

Bw.Amosi Petro ni mkazi wa Engusero amesema kuwa kutokana na ubovu wa barabara, gharama za usafiri zimepanda tofauti na hapo awali, huku wananchi wengine wakishindwa kumudu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Engusero Bi.Theresia Chibago amesema uongozi wa Kata unatambua changamoto hiyo, na tayari wamefikisha suala hilo kwa Halmashauri na kinachosubiriwa ni kuanza kwa vikao vya bajeti ili kupata fedha za kukarabati.

Pamoja na hayo Bi.Chibago ameiomba Halmashauri na Serikali kuu kuitazama upya Wilaya ya Kiteto kutokana na ubovu wa baadhi ya barabara uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Mwaka jana.