Dodoma FM

Mitaala mipya ni chachu ya vijana kujiajiri

4 July 2023, 7:28 pm

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wakitoa maoni yao kuhusu mitaala mipya ya elimu.Picha na Aisha Shaban.

Serikali ilitoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao juu ya maboresho ya rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na rasimu ya Mitaala ya elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu.

Na Aisha Shaban.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma wamesema maboresho katika sera na mitaala ya elimu Nchini itakuwa ni mwanzo wa kuwawezesha vijana kuhitimu masomo yao na kujiajiri bila kutegemea ajira kutoka serikalini.

Wametoa maoni yao wakati wakizungumza na Dodoma Tv kwa nyakati tofauti ikiwa ni majuma kadhaa yamepita tangu serikali ilipotoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao juu ya maboresho ya sera na mtaala wa elimu nchini.

Wananchi hao wamesema maboreho ya sera ya elimu yatasaidia vijana kujifunza shughuli za ujasiriamali hivyo linapokuja swala la ukosefu wa ajira wanakuwa na mbinu za kujiinua kiuchumi.

Sauti za wananchi.
Picha ni moja kati ya mitaa ya jiji la Dodoma ambapo camera ya Dodoma Tv ilipita kuzungumza na wananchi . Picha na Aisha Shaban.

Hivi karibuni katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati akizungumza katika kongamano la maboresho ya sera na mitaala ya elimu Nchini alinukuliwa akisema yapo maeneo ambayo yataenda kufanyiwa maboresho ili kuandaa sera bora ya elimu nchini kwa kuzingatia maoni na ushauri wa wananchi.

Sauti ya katibu mkuu wizara ya elimu.

Naibu waziri wa tamisemi deogratius ndejembi akatumia fursa hiyo kwa kuahidi kusimamia utekelezaji katika uendeshaji wa shule zote zikiwemo za serikali kupitia maboresho ya sera na mitaala ya elimu nchini.

Sauti ya Naibu waziri wa tamisemi.