Dodoma FM

Kata ya majeleko yakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama

24 June 2021, 10:24 am

Na; Victor Chigwada.

Wakazi wa Kata ya Majeleko Wilayani Chamwino wameiomba Serikali kuwapelekea huduma ya maji safi na salama.

Wakizungumza na taswira ya habari wakazi hao wamesema wanakabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu sasa hali inayo walazimu akina mama wa kjiji hicho kutembea umbali mrefu kutafuta maji ambayo usalama wake ni mdogo kwa matumizi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chinangali One Bw.Stephano Kamoga amekiri kuwepo kwa tatizo la uhaba wa maji ambapo amesema katika Vitongoji 12 wanalazimika kutumia kisima kimoja hivyo ameiomba Halmashauri na wafadhili kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.

Taswira ya habari ilizungumza pia na Diwani wa Kata ya Majeleko Bw.Musa Omary yeye amesema kuwa tayari upimaji wa visima umeshafanyika katika baadhi ya maeneo na wanampango wa kuboresha kisima cha maji kilichopo Majeleko kwa kuweka mashine ya dizeli badala ya umeme wa jua.

Suala la upatikanaji wa maji Vijijini limeendelea kuwa changamoto katika baadhi ya vijiji huku mamlaka ya usimamizi wa maji Vijijini RUWASA akiendelea kupambana kutatua adha hiyo.