Dodoma FM

Vijana watakiwa kujikita katika utunzaji mazingira

3 August 2023, 2:08 pm

Taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma (DOYODO). Picha na Fred cheti

Na Fred Cheti.

Wito umetolewa kwa vijana kushiriki katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kushiriki katika kampeni mbalimbali za upandaji miti ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma (DOYODO) bwana Rajabu Nunga wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv  kuelezea nafasi ya kijana katika utunzaji wa Mazingira.

Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma (DOYODO) bwana Rajabu Nunga akiongea na Dodoma Tv. Picha na Fred Cheti.

Aidha Mkurugenzi huyo ameelezea mikakati mbalimbali katika taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma inayolenga katika  utunzaji wa mazingira.

Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma