Dodoma FM

Jamii yashauriwa kuendelea kulima na kutumia mazao jamii ya mikunde

29 May 2023, 8:33 pm

Mh. David Kihenzile Mbunge wa Mufindi Kusini na mwenyekiti wa kamati akizungumza katika mawasilisho hayo. Picha na Mariam Kasawa.

Mazao jamii ya mikunde yanatajwa kuwa na protini nzuri na bora kuliko protini nyingenezo hivyo wanahamasishwa kulima na kutumia mazao hayo.

Na Mindi Joseph.

Jamii imeshauriwa kuendelea kutumia na kulima kwa wingi mazao ya jamii ya mikunde hususan mbaazi ili kuweza kupata protini katika lishe na kuongeza thamani  mazao hayo.

Ni katika mdahalo uliowakutanisha wadau wa kilimo, taasisi ya uboreshaji wa mifumo na masoko ya kilimo AMDT, kamati ya kudumu ya bunge ya kilimo ili kuweza kuzungumzia masuala mbalimbali  kuhusiana na soko la mazao jamii ya mikunde.

Katika mawasilisho ya awali inaonesha  kuwa Tanzania inafanya vizuri sana katika soko la mazao jamii ya Mikunde Kimataifa .

Sauti ya muwasilishaji.
Baadhi ya wabunge ambao ni wa wajumbe wa kamati ya kudumu wakiwa katika mawasilisho hayo. Picha Mariam Kasawa.

Akizungumza katika uwasilishaji huo mbunge wa Mkinga Mama Salma Kikwete amesema Baadhi ya maeneo yanayo zalisha mazao ya mikunde yanasahaulika sana lakini ni sehemu ambazo zinazalisha sana mazao hayo.

Sauti ya Mama Salma Kikwete.

Nao Baadhi ya wabunge walio hudhuria katika mawasilisho hayo walikuwa na haya yakusema kuhusu uzalishaji wa mazao hayo jamii ya mikunde.

Sauti za Wabunge.