Dodoma FM

Kongwa kufuatilia miradi yote ya maji inayotekelezwa wilayani humo

9 May 2023, 4:26 pm

Mhe. Remidius Mwema alimefanya mkutano na Wananchi wa vijiji vya Sagara A na B kuhusu maboresho ya chanzo cha maji katika eneo la Sagara. Picha na Duwasa .

Miradi mingi ya maji inayo onekana kusua sua inakwamisha utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi suala ambalo haliwezi kufumbiwa macho.

Na Benadetha Mwakilabi.

Wilaya ya Kongwa imeahidi kufatiliana kufanyia kazi miradi yote ya maji inayotekelezwa wilayani humo ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji Kwa wananchi wake.

Mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel amesema hayo wakati akipokea taarifa ya idara ya maji kutoka Kwa kaimu meneja wa Duwasa Kongwa ambapo ameeleza kuwa miradi mingi ya maji inayo onekana kusua sua na kukwamisha utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi suala ambalo hawezi kulifumbia macho.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kongwa.

Pia kaimu meneja wa DUWASA wilaya Kongwa bwana Mohamed Ally Amesema kuwa miradi mingi ya maji vijijini inakwamishwa na wakandarasi Kwa kuchelewesha ukamilishaji wa miradi lakini pia ofisi yake imekuwa ikiwashauri na kuvunja mkataba Kwa wakandarasi wanashindwa kutekeleza.

Sauti ya kaimu meneja wa DUWASA.
Mh. Mwema akizungumza na wananchi wa vijiji vya Sagara A na B. Picha na DUWASA .

Nae Mheshimiwa Patrick Messo Diwani wa Kata ya Songambele ameeleza Hali ya upatikanaji wa maji katika Kata yake na changamoto wanazopitia wananchi wake za kutembea umbali mrefu kupata huduma ya maji.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Songambele .