Dodoma FM

Ukarabati wa skimu za Kilimo Ruaha wafikia asilimia 60

1 December 2020, 6:20 am

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiaji Bw.Daudi Kaali

Na,Mindi Joseph

Ukarabati wa miundombinu inayopeleka maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Ruaha Mbuyuni, Namagozi na Mlenge Pawaga Mkoani Iringa iliyoharibiwa na mafuriko katika msimu wa mvua zilizopita umekamilika kwa Asilimia (60%).

Akizungumza katika ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mapema leo jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiaji Bw.Daudi Kaali amesema ukarabati huo unaolenga kutengenza njia mpya ya maji itakayopeleka maji kwenye mashamba ya wakulima yenye urefu wa mita 600 unakaribia kukamilika halikadhalika katika skimu za pawaga njia mpya yenye urefu wa mita 800 wa kuchimba na kupanga mawe.

Katika hatua nyingine Meneja wa Mfuko wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.Reginald Diamett amesema hekta zaidi ya laki sita zinazomwagiliwa kwa sasa, katika msimu wa mavuno zaidi ya shilingi Bilioni hamsini na mbili zinatarajiwa kukusanywa ambapo Asilimia (75%) itabakia kwa wakulima na asilimia ishirini na tano (25%) ndiyo itakayochangiwa katika mfuko wa umwagiliaji kama ada ya huduma ya umwagiliji.

Aidha Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu Bi.Mary Mwangisa amesema kuwa hali hii inachangiwa na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ndani kuhusu shughuli za Tume, kuwa na uelewa pamoja na kuboresha kada mbali mbali katika sekta ya umwagiliaji, Jambo ambalo pia limechangia kupanua sekta hiyo kwa kuwapeleka watalaam wa umwagiliaji katika ngazi za mikoa na wilaya kwa lengo la kusogeza huduma ya umwagiliaji karibu na wakulima katika maeneo ya vijijini.