Dodoma FM

Sera ya Jinsia kukuza usawa wa kijinsia

9 March 2024, 5:35 pm

Picha ni Waziri Gwajima akikabidhi kitabu cha sera ya Jinsia baada ya kuzindua kitabu hicho hapo jana.Picha na Mariam Kasawa.

Waziri Dkt. Gwajima amewasisitiza wanawake kujiunga na vikundi vya maendeleo ili kutumia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau na kuwahimza kujitokeza kugombea nafasi mbalimnali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

Na Mariam Matundu.

Sera ya Jinsia na maendeleo ya Wanawake  ni muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia hasa kutokana na kuweka kipaumbele kwa ushiriki wa wanaume katika jitihada za kujenga usawa wa Kijinsia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Waziri Mkuu mh. Khassim Majiliwa katika kilele cha  maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake Machi 08, 2024 yaliyofanyika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Amesema anaamini Sera hiyo itaivusha Tanzania katika kipindi kingine kirefu katika utekelekezaji wake ili kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo na Malengo ya Dunia kuhusu usawa wa kijinsia.

Sauti ya Mh Dorothy Gwajima.
Picha ni wanawake wakicheza pamoja kusherehekea siku ya wanawake . Picha na Mariam Kasawa.

Amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake huku akiwasisitiza wanawake kulinda watoto wao pamoja na kupiga namba 116 ili kutoa taarifa za vitendo hivyo vya ukatili.

Sauti ya Mh Dorothy Gwajima.

Akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi mwenyeji wa maadhimisho hayo mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh . Rosemery Senyamule alikuwa na haya yakusema.

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.