Dodoma FM

Wizara ya kilimo yaombwa kuupa mkoa wa Dodoma kipaumbele katika upatikanaji wa mbegu bora

7 September 2021, 2:11 pm

Na;Mindi Joseph .


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Jabiri Shekimweri ameiomba wizara ya kilimo kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapewa kipaumbele katika upatikanaji wa mbengu bora za kilimo ili kutatua adha ya mbegu kwa wakulima.

Akizungumza na Taswira ya habari Mh Shekimweri amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa Mbengu kwa wakulima hivyo Wizara ya kilimo ina jukumu la kuangalia namna ya upatikanaji bora wa Mbengu za kilimo Mkoani Dodoma.

Ameongeza kuwa uwepo wa Takwimu za kilimo mifugo na uvivu ni kichocheo cha kuimarisha uchumi wa kati kwani zitasaidia katika Mtawanyo wa kilimo katika kaya laki moja na 37 za Dodoma Mjini katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima.

Aidha katika kuhakikisha uzalishaji wenye tija kwa wakulima unaongezeka serikali ina wajibu wa kuhakikisha mbengu bora zinapatikana kwa wakati na toshelezi kwa wakulima.