Njia salama za uzazi wa mpango-Makala
6 June 2024, 6:42 pm
Tafiti zinaonesha kuwa wanawake wengi hawataki kupata ujauzito tena ndani ya mwaka mmoja baada ya kujifungua.
Na Mwandishi wetu.
Wakati kila mtu ana haki ya kufanya uamuzi wake kuhusu kutumia njia za uzazi wa mpango, si kila mtu anaweza kutumia haki hiyo.
Inakadiriwa kuwa wanawake milioni 923 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati wanataka kuepuka mimba, lakini inakadiriwa kuwa wanawake milioni 218 kati ya hao hawatumii njia ya kisasa ya uzazi wa mpango.
Tafiti zinaonesha kuwa wanawake wengi hawataki kupata ujauzito tena ndani ya mwaka mmoja baada ya kujifungua lakini wengi hawajui kuwa njia za uzazi wa mpango zipo kwa ajili yao na hawashauriwi jinsi wanavyoweza kupanga na kuachana na mimba za baadaye.
Leo tunazungumza na daktari wa masuala ya afya ya uzazi kujua kuna faida gani iwapo wenza watashiriki kwa pamoja kuchagua njia za uzazi wa mpango?