Dodoma FM

Wakazi wa Mtube waeleza kunufaika na Bwawa

8 August 2023, 2:55 pm

Picha ni mkulima akifunga mashine ya kusukuma maji kutoka kwenye bwawa kwaajili ya kumwagilia. Picha na George John.

Nchi yetu imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji vya aina mbalimbali ikiwemo Mito na Maziwa, licha ya kwamba Mkoa wa Dodoma unatajwa kuwa Kame lakini umejaaliwa kuwa na Mabwawa ambayo yanatumika katika Kilimo na Mwenye macho haambiwi Tazama.

Na Mindi joseph.

Uwepo wa Bwawa la maji katika Mtaa wa Mtube Mkoani Dodoma imetajwa kuwa mkombozi wa uchumi wa Wananchi na ajira kwa Vijana.

Waswahili wanasema kama unataka mali utaipata shambani ni msemo ambao Vijana hawa wanaufanyia kazi vilivyo kwani wao wamegeukia shambani kujiinua kimaisha na kiuchumi.

Sauti za wakazi wa mtaa wa Mtube.
Picha ni bwawa hilo linalo patikana katika mtaa wa Mtube jijini Dodoma. Picha na George John.

Ama kweli Mchumia Juani hulia kivulini Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtube John Masaka anasema Bwawa hili la asili limegeuka kuwa mtaji kwa wananchi wake.

Sauti ya Mwenyekiti.