Dodoma FM

MCT yakiri kukinzana kwa sheria ya matumizi sahihi ya mitandao

28 September 2023, 4:42 pm

Picha ni nembo ya baraza la Mawasiliano Tanzania MCT.Picha na MCT.

Hali hiyo imekuwa ikikinzana  na Sheria ya haki ya kupata Taarifa  ambayo inatoa wigo kwa wananchi kuwa huru kupata taarifa ambazo hazijazuiliwa kisheria.

Na Seleman Kodima.

Pamoja na Serikali kuhimiza Matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii, Baraza la Habari Tanzania limesema bado kuna kukinzana kwa sheria.

Hii ni kufuatia sheria kuwabana wananchi wenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa kuwataka walipe gharama ya Shilingi Laki Tano kwa ajili ya Usajili.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Baraza la Habari ilitolewa leo katika kuadhimisha Haki ya upatikanaji Taarifa ambayo huadhimishwa  Septemba 28 kila mwaka, imefafanua kuwa kupitia kauli mbiu ya mwaka huu ya Umuhimu wa Mitando katika Upatikanaji wa Taarifa wamekiri suala hilo kushindika kufanyika kwa sababu ya Sheria zilipo nchini.

Aidha taarifa hiyo imeeleza hali ya upatikanaji wa taarifa  kwa sasa ambapo kufikia Septemba Mwaka huu Baraza la Habari limerekodi Matukio Mawili ya waandishi kunyimwa taarifa  huku matukio mengine yakiwanyima fursa wananchi kupata taarifa kutoka kwenye Vyombo vya habari.

Baadhi ya Matukio hayo ni pamoja na Waandishi wa Habari kutishiwa,kukamatwa na kuzuiwa kwa mijadala inayohusu Dp World.

Sauti ya Bw. Kajubi Mukajanga.

Hata hivyo Baraza la Habari limetoa Mapendekezo yenye lengo la kufanikisha Haki ya upatikanaji wa taarifa ikiwa ni pamoja mitandano ya kijamii itumike kwa umakini  katika kutoka taarifa sahihi na za ukweli,Serikali kuendelea na nia yake kufanyia marekebisho sheria mbalimbali ambazo zinakandamiza Uhuru wa Kujieleza pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.

Sauti ya Bw. Kajubi Mukajanga.

Baraza limeomba Serikali iendelee kusikiliza maoni ya Wadau na kuyafanyia kazi  kutazama upya sheria ya EPOCA katika kanuni za mtandaoni ,Sheria ya haki ya  kupata taarifa  2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni zinafanyiwa marekebisho ambayo yatachangiza upatikanaji rahisi wa taarifa kwa wananchi.